Tuesday, August 9, 2011

Waziri wa Mambo ya Kigeni: Cuba inaunga mkono haki ya Palestina kuwa taifa huru


Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Cuba Bwana Bruno Rodriguez

HAVANA--- Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Cuba Bwana Bruno Rodriguez, amesisitiza kuwa nchi yake itaiunga mkono Palestina, ambaye ni rafiki yake wa siku nyingi katika mapambano ya kupigania uhuru ili iwe taifa huru.
Aliyasema hayo jana katika mkutano wake na Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Palestina Bwana Riyad Al-Malki, katika makao makuu ya wizara ya mambo ya kigeni ya Cuba.
Bw. Rodriguez alimhakikishia mgeni wake kuwa Cuba itafanya kila linalowezekana kuhakikisha kuwa Palestina inapata utaifa wake kwa mujibu wa mipaka ya mwaka 1967 na ya kwamba Jerusalem mashariki itakuwa makao yake makuu.
Itafanya hivyo kwa kupiga kura ya ndiyo kwenye kikao kijacho cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwezi Septemba.

No comments:

Post a Comment