Tuesday, August 9, 2011
Sri Lanka yaiunga mkonon Palestina kujiunga na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa
COLOMBO---Waziri mdogo wa Mambo ya Kigeni wa Sri Lanka Bwana Gamini Peiris, jana alithibitisha kuwa nchi yake itaunga mkono mpango wa Mamlaka ya Palestina (PA) kuomba uanachama wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwezi Septemba.
Bw. Peiris aliyasema hayo alipokutana na balozi wa Palestina nchini Sri Lanka na Maldives, Bwana Anwar al-Agha.
Alisema nchi yake itaiunga mkono Palestina ili ipate utaifa wake, ikiwa na Jerusalem kama makao yake makuu.
Bw. Al-Agha alimfahamisha mwenyeji wake Bwana Peiris juu ya maendeleo huko Palestina na mazungumzo kati yake na serikali ya Israeli, ambayo yamevunjika kutokana na kiburi cha nchi hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment