Balozi Job Lusinde, alikuwa waziri wa kwanza kabisa katika Baraza la Mawaziri wa serikali ya kwanza ya Tanganyika baada ya uhuru mwaka 1961 (kulia) akiwa na aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Morogoro Bwana Stphen Masishanga (kushoto)
MZEE wa siku nyingi na aliyekuwa waziri wa kwanza katika Baraza la Mawaziri la serikali ya kwanza ya Jamhuri ya Tanganyika ikiongozwa na hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Balozi Job Lusinde amesema kuwa serikali ya awamu ya nne ikiongozwa na Rais Jakaya Kikwete imeshindwa kusimamia rasilimali za nchi na hivyo kuididimiza nchi hii katika lindi la umaskini.
Aliyasema hayo jana katika mahojiano maalumu na mwandishi wa TBC Joseph Bura katika kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika (sasa TANZANIA).
Aliongeza kusema kuwa hali za wananchi zimedidimia kiuchumi, mashirika mengi, akayataja Shirika la Reli Tanzania, Shirika la Ndege Tanzania na Shirika la Bandari Tanzania kuwa yamefilisika na kwamba wananchi wana taabika kukosa usafiri wa uhakika.
"Ingawa tumefanya vizuri katika sekta zingine za miundombinu hasa barabara, elimu nk, bado huduma za afya ni mbaya sana na zinahitaji kuboreshwa zaidi," alisema.
Aliongeza kusema kuwa ikiwa huduma za reli zitaimarika na barabara ya Iringa hadi Arusha, basi Dodoma itakuwa imefunguka na itapata unafuu mkubwa wa kibiasharana na kufikika kwa urahisi zaidi.
Akaishauri serikali hii kuacha kuwalinda mafisadi na badala yake ikomeshe rushwa ili jamii iwe na imani nayo.


No comments:
Post a Comment