Friday, August 26, 2011
SAKATA LA JENGO LA TGNP, MABIBO JIJINI DAR ES SALAAM
Bi Usu Malya, mkurugenzi mtendaji wa TGNP
MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP) ni mmiliki halali wa jengo lenye hati namba 56998, Kiwanja namba 22/3/1 lililoko katika eneo la Mabibo Dar es Salaam
Mtandao wa Jinsia ulinunua jengo hilo kutoka kwa Mfilisi (Benki ya Rasilimali Tanzania- TIB) kwa iliyokuwa Tanzania Sewing Thread Manufacturers Limited ambayo ilikuwa sehemu ya kampuni tanzu ya Tanzania Textile Company Limited (TEXCO) kwa gharama ya shilingi milioni 200 ambapo makubaliano ya manunuzi yalifanyika tarehe 15/6/ 1997.
Mchakato wa uuzaji wa jengo hili ulikuwa wa wazi uliotangazwa katika vyombo vya habari nchini hususan magazeti.
Baadhi ya watumiaji wa ofisi waliokuwa ndani ya jengo hilo wakati TEXCO ikiwa inafilisiwa nao walishiriki katika mchakato wa kununua bila mafanikio.
Baada ya TGNP kushinda ‘tender’, baadhi ya watumiaji hao , mnano mwezi wa Julai 1997 walifungua kesi namba 215 / 1997 dhidi ya TIB kama mshitakiwa wa kwanza na TGNP mshitakiwa wa pili katika mahakama kuu kupinga maamuzi ya TIB kuiuzia TGNP jengo hilo.
UAMUZI WA MAHAKAMA KUU
Kesi hii ilichukua muda mrefu sana takribani miaka kumi na mbili mpaka kufikia tarehe 15/10/ 2009, uamuzi wa Mahakama Kuu ulipotolewa na Mheshimiwa Jaji T.B. Mihayo.
Mahakama Kuu ilitowa hukumu ambayo iliwapa haki TGNP na kuwaamuru walalamikaji kuondoka mara moja na kulipa gharama za kesi.
Wakati mchakato wa kutekeleza hukumu ya Mahakama Kuu ukiendelea, tarehe 19/9/2009 walalamikaji walipeleka katika Mahakama ya Rufaa azimio la kusimamisha utekelezaji wa hukumu ya mahakama kuu ya kuwatoa kwenye jengo kwa kupitia ombi na 129 la 2009.
Ombi lao hilo lilitupiliwa mbali na Mahakama ya Rufaa tarehe 23/8/2011.
MCHAKATO WA KUTEKELEZA UAMUZI WA MAHAKAMA
TGNP,ambao ndio wamiliki halali wa hili jengo hilo tunasubiri utekelezaji wa uamuzi wa Mahakama ya Rufaa iliyotolewa terehe 23/8/2011.
Tutaendelea kuwataarifu maendeleo ya mchakato huu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment