Tuesday, August 23, 2011

Thailand kuunga mkono taifa la Palestina


Thailand's foreign minister Mr Kasit Piryoma
Thailand imesema itaunga mkono kuundwa kwa taifa la Palestina kura itakapopigwa kwenye Baraza Kuu la Umoja mwezi Septemba mwaka huu.
Hayo yamesemwa na Bwana Nabil Shaath, mjumbe wa Kamati Kuu ya Utendaji ya Chama cha Fatah.
Shaath alifanya mazungumzo na waziri wa mambo ya kigeni wa Thailand Kasit Piryoma.
Palestina ina mpango wa kutaka Umoja wa Mataifa kuitambua Palestina kama mwanachama aliye nchi huru ikiwa na mipaka yake kama ilivyokuwa mwaka 1967.
Thailand imekubali kupiga kura kuiunga mkono kupata uanachama wa Umoja wa Mataifa.
Kiongozi huyo wa Fatah yuko safarini nchi za nje kutaka kuungwa mkono kwa taifa la Palestina kwenye chombo hiki muhimu cha kimataifa.

No comments:

Post a Comment