Wednesday, July 27, 2011
Umuhimu wa 'kazi' kwa maisha ya binadamu
Kazi ni sehemu isiyotengeka ya maisha ya mwanadamu. Allah Mtukufu ameifanya kazi kuwa ndio wasila wa mwanadamu katika kupata maisha (riziki) yake ulimwenguni hapa. Tusome huku tukitafakari. “YEYE NDIYE ALIYEFANYA ARDHI IWE INAWEZA KUTUMIKA (Kwa kila myatakayo) KWA AJILI YENU. BASI NENDENI KATIKA PANDE ZAKE ZOTE NA KULENI KATIKA RIZIKI YAKE, NA KWAKE YEYE NDIO MAREJEO (yenu nyote)” (67: 65).
Kwenda katika pande (sehemu/nchi) za ardhi hili ni suala la kushughulika na kuhangaika kwa ajili ya kutafuta maisha. Mitume wa Allah-Rehema na Amani ya Allah iwashukie – ambao ndio Waalimu wateule wa Allah kwa waja wake, pia nao walishiriki katika kufanya kazi. Hawa Allah asingeshindwa kuwaruzuku bila ya kufanya kazi. Lakini aliwataka wafanye kazi ili wawe ni mfano mwema wa kuigwa na sisi wafuasi wao. Pia ili kuonyesha kwamba kila mmoja. Hana budi kula kupitia jasho lake.
Huyu hjapa Nabii Daudi mfanyakazi:”….NA TUKAMLAINISHA CHUMA. (Tukamwambia). TENGENEZA (nguo za chuma) PANA NA UPIME VIZURI KATIKA KIUNGANISHA, NA FANYENI VITENDO VIZURI…….” (34:10-12)
Aya inatubainishia kwamba Nabiii Daudi – Amani ya Allah imshukie – alikuwa ni fundi muhunzi akitengeneza na kuuza mavazi ya chuma ambayo yalikuwa yakitumika vitani. Tena Allah, anamuagiza aifanya kazi yake hiyo kwa ufanisi mkubwa. Bwana Mtume – Rehema na Amani zimshukie analisisitiza suala hili la ufanisi kazini katika kauli yake: Hakika Allah anapenda mmoja wenu afanyapo kazi, basi aifanya kwa ukamilifu/uzuri (ufanisi) Al-baihaqiy). Ione nafasi ya kazi katika uislamu kupitia aya hii, tusome na tutafakari pamoja." NA ITAKAPOKWISHA SWALA (kuswaliwa) TAWANYIKENI KATIKA ARDHI MTAFUTE FADHILA ZA ALLAH……….” (62:10).
Nae Bwana Mtume Rehema na Amani zimmiminikie – anasema katika hadithi – Qudsi: “ Hakika Allah anasema: Ewe mja wangu wee! Utikise mkono wako nikuteremshie riziki.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment