Wednesday, July 27, 2011

Sheikh wa Al-Azhar akiri: Hosni Mubarak, alikuwa akiwalazimisha Maulamaa kuwakufurisha Mashia.


Sheikh Ahmed al- Tayyib

Ahmed al-Tayyib, Sheikh marufu wa al-Azhar amesema kuwa dikteta aliyeondolewa madarakani nchini Misri hivi karibuni, Hosni Mubarak alikuwa akiwalazimisha maulamaa wa Misri kutoa fatuwa za kuwakufurisha Waislamu wa madhehebu ya Shia kwa shabaha ya kuzusha khitilafu na ugomvi baina ya Shia na Sunni na kuuridhisha utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.

Sheikh wa al Azhar amefichua baadhi ya jinai hizo za Rais wa zamani wa Misri katika kikao chake na wanaharakati wa chama al Nasiri mjini Cairo. Sheikh Ahmed Al-Tayyib amesema:

"Hosni Mubarak alinitaka mara kadhaa nitoe fatuwa kali dhidi ya Mashia na Hizbullah ya Lebanon lakini nilikataa kufanya hivyo licha ya mashinikizo makali."

No comments:

Post a Comment