Tuesday, July 19, 2011

'Syria yaitambua Palestina kama taifa kwa mujibu wa mipaka ya 1967'


Syrian foreign minister Farouq al- Sharaah


DAMASCUS-- Syria imetangaza kuwa inaitambua Palestina kama nchi huru kwa mujibu wa mipaka ya mwaka inayojumuisha Ukingo wa Magharibi na Uwanda wa Gaza, makao yake makuu ni Jerusalaemu ya mashariki, taarifa kutoka wizara ya mambo ya kigeni ya nchi hiyo imesema.
Taarifa imesema: “Utambuzi huu umekuja kuhakikisha haki ya Wapalestina inapatikana kikamilifu na kwamba kuonewa kunako fanywa na majeshi ya Israeli kwa wananchi wa Palestina kunakoma mara moja.”
Imeongeza kusema kuwa Ofisi ya Chama cha Wapigania Uhuru wa Palestina (PLO) iliyoko mjini Damascus imekuzwa na kuwa ofisi kamili ya ubalozi wa Palestina.
Chama cha PLO kina mipango ya kulitaka baraza kuu la Umoja wa Mataifa kuitambua Palestina kama taifa huru kwenye kikao chake cha mwezi Septemba mwaka huu, ikiwa mazungumzo ya kutafuta suluhu ya mzozo huo itashindikana.
Hata hivyo Israeli na Marekani zinapinga mpango huu wa Palestina.
Uanachama wa Palestina kwenye umoja wa mataifa unatarajiwa kuombwa na Jumuia ya nchi za Kiarabu (Arab League.)

No comments:

Post a Comment