Thursday, July 28, 2011

'Askari wa Israeli waliwatia mbaroni wanaharakati saba'



Israeli atrocities to Palestinians unattainable



Askari wa Israeli waliwatia mbaroni wanaharakati saba waliokuwa wakishiriki katika maanadamano huko Al-Walaja, jana asubuhi.
Bwana Ala Ad-Deras, mjumbe wa kamati ya Kupinga Ukuta wa Kibaguzi alisema askari hao waliwatia mbaroni wanaharakati saba, wakiwemo wageni watano.
Ardhi ya kijiji kilichoko kaskazini mwa mji wa Bethlehem, pia iliharibiwa vibaya na uvamizi huo wa askari wa Israeli.
Askari hao mara nyingi huzua ghasia na fujo kwa wananchi bila sababu ya msingi, kitendo kilichosababisha maanadamano kuzuka huko, Ad-Deras.

Askari hao wanaripotiwa pia kuharibu ardhi kadhaa ya wanakijiji kwa kung’oa miti ya matunda na misonobari.
Bwana Awad Abu Sway, msemaji wa wizara ya kilimo alisema askari hao waliharibu barabara inayoelekea kwenye mti wa kihistoria wa mzeituni wenye umri wa miaka 5,000.
Barabara hiyo ilijengwa kwa ufadhili kutoka nje.

No comments:

Post a Comment