Wednesday, July 20, 2011
'MGANGA WA KIENYEJI TABORA ATOWEKA NA SEHEMU ZA SIRI ZA MGONJWA WAKE'
Katika hali ambayo si ya kawaida kabisa, mganga mmoja wa kienyeji, maarufu 'sangoma' ametoweka na nyeti za mgonjwa wake wa kike baada ya kuzifyeka na kisu.
Tukio hilo lilitokea Julai 6, mwaka huu majira ya saa moja usiku katika kijiji cha Mwendakulima, huko Urambo mkoani Tabora baada ya mganga huyo kumdanganya mgonjwa wake kwamba ni lazima amchanje chale sehemu za siri ili apone, kwa kuwa alikuwa amerogwa.
Ghafla, alimkata sehemu hizo na kukimbia nazo kusikojulikana hadi sasa.
Habari za uhakika kutoka Urambo zilizothibitishwa na kamanda wa polisi mkoa wa Tabora, Liberatus Barlow, zilieleza kwamba, mwanamke huyo alifariki dunia kutokana na kuvuja damu nyingi.
Alikatwa na mganga huyo, kwa madai kuwa ya kumponya ugonjwa uliokuwa ukimsumbua kwa muda mrefu.
Juhudi za kumsaka mganga huyo zinaendelea.
Polisi wamethibitisha kumsaka mganga huyo kwa udi na uvumba ili afikishwe katika vyombo vya sheria, kwa kitendo chake hicho cha kinyama.
Kamanda Barlow ametoa wito kwa wananchi mkoani Tabora kutoa taarifa polisi kuhusu watu kama hao, ambao wanajifanya waganga kumbe ni matapeli wenye lengo la kujipatia utajiri kwa njia za haramu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment