Wednesday, July 20, 2011
Muuguzi afanya ‘madudu' hospitali ya Kitete, Tabora
Kazi ya uuguzi ni ya wito, ifanyike kwa umakini ili kuokoa maisha ya wagonjwa
HOSPITALI ya Mkoa wa Tabora, Kitete, imeingia kwenye kashfa baada ya mmoja wa manesi wa zamu kudaiwa kufanya uzembe uliosababisha mzazi kujifungua na mtoto kuanguka sakafuni.
Tukio hilo la kuhuzunisha limetokea mjini Tabora juzi.
Mama Neema Godwin, (32), aliyeomba msaada wakati akijifungua na kushindikana na hivyo mtoto kuanguka sakafuni na mama kuzirai.
Akisimulia mkasa huo, Neema, mkazi wa Kata ya Chemchem, Manispaa ya Tabora alisema siku ya tukio alipatwa na uchungu na kufikia hatua ya kujifungua na kuomba nesi wa zamu ampime.
“Nilimuomba nesi huyo kuja kunipima anisaidie kwani niliona kuwa wakati umefika wa kujifungua lakini aligoma na kusema kuwa mimi muda bado mbona ni msumbufu,”
Anasema badala yake nesi huyo aliendelea na kazi zake, “Niliporudia tena kumuita alinieleza tena niache kelele na akaniambia ninyanyuke niende pale alipo haraka…niliamka na kuanza kumfuata kabla sijapiga hata hatua moja chupa ilipasuka na nikaamua kurudi kitandani.
“Nilipoona amekataa nilishitukia tu mtoto ametoka na kudondoka chini na hapo nilipiga kelele tena kwa kumwambia nesi huyo kuwa amekataa kuja na mtoto ametoka na kama atakufa hatokubali, ndipo nesi huyo aliopokuja mbio kumchukua mtoto huyo.” alisema.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Kitete, Mkoa wa Tabora, Dk Lesley Mhina alikiri kuwapo kwa tukio hilo na kubainisha tayari uchunguzi umefanyika na hatua za kinidhamu zimeanza kuchukuliwa.
“Nilipopata taarifa hizi za kinyama, niliunda tume kwani nilikuwa safarini na kubaini kuwa tukio hilo lilikuwepo na tayari wahusika wote nimewatwanga barua nina imani hatua zaidi zitachukuliwa.
“Mimi binafsi nimesikitishwa na tukio hili na nimeanza kuchukua hatua kali ili hapa hospitalini kwangu tabia hii niikomeshe, wazazi wamekuwa wakilalamika mara nyingi, nataka kukomesha zaidi isijirudie, alisema Mganga huyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Huo ni unyama, upigwe vita
ReplyDelete