Tuesday, May 31, 2011

POLISI YAFANYA MAUAJI YA KUTISHA TABORA

POLISI YAFANYA MAUAJI YA KUTISHA:

*Baada ya Arusha, Nyamongo sasa Tabora!

TAARIFA iliyotolewa jana na Kamamda wa Polisi mkoa wa Tabora, Bwana Liberatus Barlow imethibitisha, bila kificho walas haya, kuwa polisi imewatwanga risasi watu wawili na kufa papo hapo na wengine wengi wako hoi walikolazwa katika hospitali ya mkoa-Kitete.
Sababu hasa za mauaji hayo ni kwa polisi hao kufanya uvamizi wa maksudi kwenye mkutano wa hadhara ulioitiswa na viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF), akiwemo mbunge wa viti maalum, Magdalena Sakaya; kupinga kile kilchoitwa ‘unyama’ uliofanywa na polisi hao kwa wananchi wa kubomolewa makazi yao na kunyang’anywa mifugo wao, kwa kisingizio eti ‘kuishi katika eneo la hifadhi.’
Huu ni unyama mwingine unaofanywa na vyombo vya dola kwa maksudi ‘impunity’ dhidi ya wananchi wasiokuwa na hatia yoyote ile na ambao hawamiliki silaha za aina yoyote ile.
Kosa lao ni kuishi katika hifadhi, ndiyo maana wanauliwa kama swala. Heri ya mnyama anaheshimiwa kulikoni mwanadamu, utu wake na mali zake hazina thamani tena.
Mpaka sasa, katika mwaka huu pekee, polisi wameua raia wengi sana, yasemekana wanafikia 82 kwa maksudi na hatuoni hatua yeyote ile ikichukuliwa dhidi ya askari au jeshi la polisi kwa ujumla.
Suali la kujiuliza, je, misingi ya sheria katika nchi hii inalindwa au mambo yanakwenda ovyo tu?
Tunaomba mauaji haya ya Tabora yachunguzwe na hatua zichukuliwe dhidi ya polisi hawa wauaji...!
………………………………………………………………………………………………………

1 comment:

  1. Hii kali tena, kwa polisi wetu kuwa wauaji wa raia wema.
    Je, kazi yao ni nini hasa? Au ni kuua watu tu, basi.
    Tabia hii iachwe ikiwa tunataka kujenga taifa linalofuata misingi ya demokrasia na utawala bora.

    ReplyDelete