Netanyahu: Vunjeni makubaliano na Hamas
WASHINGTON – WAZIRI mkuu wa Israeli Bwana Benjamin Netanyahu aliliambia Baraza la Congress la Marekani kuwa atayaondoa makazi ya walowezi ikiwa tu kutakuwa na makubaliano ya kweli ya amani na Wapalestina.
Lakini akakataa katakata matakwa ya jumuia ya kimataifa yanayoitaka nchi hiyo kurejesha ardhi iliyoikwapua hadi kufikia mipaka ya mwaka 1967 au kuugawana mji wa Jerusalem.
Netanyahu pia alikataa kurejea kwenye meza ya mazungumzo kati yake na Rais wa Palestina Bwana Mahmoud Abbas huku kukiwa na Chama cha Hamas.
Netanyahu pia alikataa kurejea kwenye meza ya mazungumzo kati yake na Rais wa Palestina Bwana Mahmoud Abbas huku kukiwa na Chama cha Hamas.
Akaongeza kusema kuwa jambo ambalo linakwamisha kufikiwa kwa amani ya kudumu ya mzozo huo ni kukataa kwa Wapalestina kuitambua Israeli.
"Tutakuwa wema juu ya ukubwa wa taifa la Palestina," alisema huku akishangiliwa na wajumbe wa Baraza hilo.
"Tutakuwa wema juu ya ukubwa wa taifa la Palestina," alisema huku akishangiliwa na wajumbe wa Baraza hilo.
Wapalestina kwa upande wao wanataka Jerusalemu ya Mashariki iwe mji wao mkuu wa taifa jipya la Palestina.
"Kwa kusema ukweli Jerusalem haiwezi kugawanywa tena. Jerusalem inabaki mji mkuu wa taifa la Israeli," Netanyahu alisema.
Obama, wiki iliyopita alisema Marekani na Jumuia ya Kimataifa wanataka taifa la Palestina liundwe kulingana na mipaka ya iliyokuwepo kabla ya vita ya siku sita ya mwaka 1967.
Obama, wiki iliyopita alisema Marekani na Jumuia ya Kimataifa wanataka taifa la Palestina liundwe kulingana na mipaka ya iliyokuwepo kabla ya vita ya siku sita ya mwaka 1967.
Wapalestina waikataa hotuba ya Netanyahu
ReplyDeleteRAMALLAH—MSEMAJI wa raisi Nabil Abu Rudeineh amesema kile ambacho Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu alikisema kwenye Bunge la Marekani wiki hii haitaleta amani.
“Kile ambacho Netanyahu amekisema katu hakitaleta amani,” alisema na kumshutumu waziri mkuu huyo kuwa ni kikwazo cha kufikia amani ya kweli.
“Amani kwetu sisi ni kuwepo kwa taifa huru la Palestina kwa mujibu wa mipaka ya mwaka 1967, ikiwa na Jerusalemu ya Mashariki kama mji wake mkuu,” alisema Abu Rudeineh.
Pia aliongeza kusema: “Kamwe hatutakubali kuwepo na Muisraeli yeyote katika ardhi ya Palestina, hasa katika Ukanda wa mto Jordan.”
Alisema amani iwe ni kwa mujibu wa maazimio ya kimataifa na makubaliano na siyo kuweka masharti na mapingamizi.
Wakati huo huo, Nabil Shaath, msaidizi wa raisi Abbas, alisema matamshi ya Bwana Netanyahu ni tangazo la vita dhahiri na Wapalestina.