Tuesday, May 31, 2011

POLISI YAFANYA MAUAJI YA KUTISHA TABORA

POLISI YAFANYA MAUAJI YA KUTISHA:

*Baada ya Arusha, Nyamongo sasa Tabora!

TAARIFA iliyotolewa jana na Kamamda wa Polisi mkoa wa Tabora, Bwana Liberatus Barlow imethibitisha, bila kificho walas haya, kuwa polisi imewatwanga risasi watu wawili na kufa papo hapo na wengine wengi wako hoi walikolazwa katika hospitali ya mkoa-Kitete.
Sababu hasa za mauaji hayo ni kwa polisi hao kufanya uvamizi wa maksudi kwenye mkutano wa hadhara ulioitiswa na viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF), akiwemo mbunge wa viti maalum, Magdalena Sakaya; kupinga kile kilchoitwa ‘unyama’ uliofanywa na polisi hao kwa wananchi wa kubomolewa makazi yao na kunyang’anywa mifugo wao, kwa kisingizio eti ‘kuishi katika eneo la hifadhi.’
Huu ni unyama mwingine unaofanywa na vyombo vya dola kwa maksudi ‘impunity’ dhidi ya wananchi wasiokuwa na hatia yoyote ile na ambao hawamiliki silaha za aina yoyote ile.
Kosa lao ni kuishi katika hifadhi, ndiyo maana wanauliwa kama swala. Heri ya mnyama anaheshimiwa kulikoni mwanadamu, utu wake na mali zake hazina thamani tena.
Mpaka sasa, katika mwaka huu pekee, polisi wameua raia wengi sana, yasemekana wanafikia 82 kwa maksudi na hatuoni hatua yeyote ile ikichukuliwa dhidi ya askari au jeshi la polisi kwa ujumla.
Suali la kujiuliza, je, misingi ya sheria katika nchi hii inalindwa au mambo yanakwenda ovyo tu?
Tunaomba mauaji haya ya Tabora yachunguzwe na hatua zichukuliwe dhidi ya polisi hawa wauaji...!
………………………………………………………………………………………………………

Wednesday, May 25, 2011

NETANYAHU NI KIKWAZO CHA AMANI NA WAPALESTINA


Netanyahu: Vunjeni makubaliano na Hamas

WASHINGTON – WAZIRI mkuu wa Israeli Bwana Benjamin Netanyahu aliliambia Baraza la Congress la Marekani kuwa atayaondoa makazi ya walowezi ikiwa tu kutakuwa na makubaliano ya kweli ya amani na Wapalestina.
Lakini akakataa katakata matakwa ya jumuia ya kimataifa yanayoitaka nchi hiyo kurejesha ardhi iliyoikwapua hadi kufikia mipaka ya mwaka 1967 au kuugawana mji wa Jerusalem.
Netanyahu pia alikataa kurejea kwenye meza ya mazungumzo kati yake na Rais wa Palestina Bwana Mahmoud Abbas huku kukiwa na Chama cha Hamas.
Akaongeza kusema kuwa jambo ambalo linakwamisha kufikiwa kwa amani ya kudumu ya mzozo huo ni kukataa kwa Wapalestina kuitambua Israeli.
"Tutakuwa wema juu ya ukubwa wa taifa la Palestina," alisema huku akishangiliwa na wajumbe wa Baraza hilo.
Wapalestina kwa upande wao wanataka Jerusalemu ya Mashariki iwe mji wao mkuu wa taifa jipya la Palestina.
"Kwa kusema ukweli Jerusalem haiwezi kugawanywa tena. Jerusalem inabaki mji mkuu wa taifa la Israeli," Netanyahu alisema.
Obama, wiki iliyopita alisema Marekani na Jumuia ya Kimataifa wanataka taifa la Palestina liundwe kulingana na mipaka ya iliyokuwepo kabla ya vita ya siku sita ya mwaka 1967.


MIUNDO MBINU YA BARABARA TANZANIA NI MIBOVU KABISA

Kwa muda mrefu sasa, Tanzania haijakuwa na miundo mbinu mizuri ya barabara kama inavyohitajika. Miaka 49+ ya uhuru wa Tanganyika haijaleta matunda mazuri kwa wananchi wake. Hali ya maisha ni mbaya, uchumi ni mbovu na wananchi wake wanazidi kuwa maskini tu, huku ufisadi ukiota mizizi katika kila nyanja ya maisha. Leo hii kwenda Gongo la Mboto mathalani, au Mbezi; mtu humchukua saa mbili nzima kutokana na foleni au msongamano wa magari ulivyo kwa kuwa barabara ni mbaya, hazikidhi haja hata kidogo. Je, viongozi wetu hawalioni hilo?

KUHUSU: TANESCO imeshindwa kutatua tatizo la UMEME Tanzania

KWA muda mrefu sasa, Shirika la ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO) limeshindwa kabisa kutatua tatizo la muda mrefu ambalo limeikumba nchi hii kwa kuwa uwajibikaji wake ni mdogo. Kinachotakiwa sasa ni kwa serikali kufungua milango kwa wawekezaji kutoka nchi za nje na pia kwa wazalendo ambao wana uwezo wa kuzalisha, kusambaza na kuuza umeme kwa wananchi kwa bei nafuu ili tatizo hili liweze kumalizika kabisa.