SERIKALI ya mapinduzi ya Zanzibar imeukataa msaada wa maafa uliokuwa utolewe na kampuni ya simu za mikononi ya VODACOM kufuatia wananchi kuilalamikia kampuni hiyo kuendesha mashindano ya miss Tanzania wakati Wazanzibari wapo katika msiba wa kitaifa.
Waziri wa nchi ofisi ya makamo wa pili wa rais Mohamed Aboud alithibtisha kuwepo kwa taarifa hizo za SMZ kukataa msaada wa maafa uliokuwa utolewe na kampuni ya simu ya mikononi ya VODACOM.
'Ni kweli tumekataa kupokea msaada huo ingawa hatujuwi ni kiasi gani cha fedha....unajuwa wananchi wengi wametoa malalamiko yao na kukerwa kwa wafadhili hao wa mashindano ya urembo kuendelea na unesho lao wakati huku taifa limepatwa na msiba mkubwa'alisema Aboud.
Alisema wadhamini hao walikuwa wanatakkiwa kufahamu wajibu wao kwa jamii zaidi wakati inapokutwa na maafa kama hayo ya kuzama kwa meli na wananchi zaidi 197 kupoteza maisha yao.
Aboud alisema haielekei hata kidogo kwa kampuni hiyo iliyodhamini mashindano hayo kuendelea wakati huku rais wa jamhuri ya muungano Jakaya Kikwete ametangaza msiba wa taifa pamoja na rais wa Zanzibar dk.Ali Mohamed Shein.
Wananchi wengi wa Zanzibar walikerwa na kitendo cha kuendelea kufanyika kwa maonesho ya urembo ya kumtafuta miss wa Tanzania katika kipindi ambapo taifa lipo katika msiba mkubwa.
No comments:
Post a Comment