Monday, October 3, 2011

‘WAMATO chatoa huduma ya ARVs kwa wagonjwa wa UKIMWI Mbezi Beach’

Mama Basila Chuwa, Mwenyekiti wa WAMATO huko Mbezi Beach

Na Nasser Kigwangallah
KIKUNDI cha Akina Mama na Watoto (WAMATO) cha Mbezi Beach jijini Dare s salaam, ni miongoni mwa vikundi ambavyo hutoa huduma za kijamii kwa kuwasaidia watoto, akina mama na wajane ambao kwa namna moja au nyingine wameachwa na wazazi wao au waume wao waliofariki kutokana na ugonjwa wa UKIMWI.
Hivi sasa kikundi hicho kinatoa chakula, dawa za kurefusha maisha (ARVs), elimu n huduma za fya kwa wagonjwa wa UKIMWI wapato sitini hivi; wanake na wanaume khmsini n watoto kumi katika eneo la Mbezi Beach.
Hizi ni juhudi za kupongezwa sana na zinapaswa kuungwa mkono na wasamari wema hapa jijini na nchini kote kwa ujumla.
Pia WAMATO inaendesha shule ya awali na msingi hapo hapo Mbezi Beach, kwa kusomesha wanafunzi kutoka familia za kimaskini wa eneo hilo.
Shule hiyo, inayoitwa kwa jina la Bajeziro; ina wanafunzi mia tatu na tayari imesomesha wanafunzi elfu moja na mia mbili toka kuanziswa kwake miaka kumi iliyopita.
Wengi wa wanafunzi hao hivi sasa wako katika shule za sekondari na wengine wako chuo kikuu.
WAMATO inafadhiliwa na shirika moja la Canada ambalo limesema litasitisha msaada wake kwa kikundi hicho ifikapo mwezi Machi mwaka kesho kwa kuwa limekuwa mfadhili wake mkuu kwa takriban miaka kumi sasa.
“Kutokana na kukoma ufadhili wake huo, WAMATO sasa iko njia panda, haijui itawasaidia vipi akina mama na watoto wanoishi na virui vya UKIMWI na pia kutoa huduma ya chakula, dawa na sare za shule kwa watoto yatima, ambao wengi wao ni maskini sana,” anasema Mama Basila Chuwa, Mwenyekiti Mtendaji wa WAMATO.
Anaongeza kusema kuwa wagonjwa ambao anawahudumia hivi sasa ni maskini mno, hawajiwezi kwa lolote na hapana budi kuendelea kuwasaidia ili maisha yao yaweze kuimarika.
Anasema na kama hatopata msaada wa kutoha kutoka serikalini, mashirika ya kijamii na wahisani mbalimbali wa ndani na nje; bila shaka huduma zake za kutoa chakula, dawa na elimu bure kwa watoto yatima, maskini na wale wanaoishi katika mazingira magumu zitazorota.
Akizungumza kwa uchungu sana, Maria Magdlena Hasara (umri miaka 65) mama anayeishi kwa UKIMWI na kupewa msaada wa chakula, dwa n matibabu mengine kutoka WAMATO, anasema hali yake sasa imeimarika kutokana na msaada huo.



Anasema alipata UKIMWI miaka mitatu iliyopita kutoka kwa binti yke aliyekuwa na ugonjwa wa ukimwi na kupata uja uzito.
Alimsaidia kujifungua, bahati mbya ana hakutumia mipira wakati akimsaidia kujifungualia nyumbnani.
“Toka wakati huo, hali yangu ilibadilika ghafla na kujikuta nikiwa nimeambukizwa UKIMWI,”anasema.
Anongeza kusema kuwa kwa msaada wa WAMATO, hali yake ni nzuri na analea wajukuu sita, wawili wa huyo binti yake ambaye alifariki dunia mwaka 2007 na kumwachia watoto wawili; Tausi (15) na Neema (3)na wengine wanne ni watoto wa ndugu zake ambao nao wamekufa kwa ukimwi.
Maisha ya bibi huyu ni magumu sana. Anaishi kwa kugonga kokoto na wajukuu zake hao wanamsaisdia, hivyo maisha yanakwenda.
Na bila ya msaada wa WAMATO sijui hali yake leo ingekuwaje?
Kwani WAMATO wanamsaidia chakula, dawa na elimu kwa wajukuu zake hao, zikiwemo sare za shule.